Wilaya ya Ludewa ni wilaya mojawapo kati ya 6 za Mkoa wa Njombe.
Ludewa iko upande wa kaskazini-mashariki ya Ziwa Nyassa. Wilaya imepakana na wilaya za Njombe na Makete, upande wa mashariki na mkoa wa Ruvuma na upande wa kusini na nchi ya Malawi ng'ambo ya ziwa.
Makao makuu ni mji wa Ludewa.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 151,361 [1]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 128,520 [2].
Wenyeji asilia wa Ludewa ni Wapangwa, Wakisi na Wamanda.
Karibu na Lugarawa akiba kubwa ya mtapo wa chuma imetambuliwa kuna mpango wa kuanzisha migodi ya Liganga. Akiba ya madini za chuma ni zaidi ya tani bilioni 1 na hivyo akiba kubwa inayojulikana Afrika. Kuna mradi wa kampuni ya Kichina Sichuan Hongda Group Ltd inayotaka kuzalisha feleji kwa kutumia makaa kutoka akiba ya Mchuchuma karibu na Ziwa Nyasa[3]