Yatima (kwa Kiingereza orphan, kutoka Kigiriki ορφανός, orfanós[1]) ni mtoto aliyefiwa au kutelekezwa moja kwa moja na wazazi wake wote[2][3]. Kwa kawaida mtoto aliyewapoteza wazazi wake wote wawili anaitwa yatima.
Watu wazima pia wanaweza kuitwa mayatima. Ingawaje, watu waliofikia utu uzima kabla wazazi wao hawajafariki kwa kawaida hawaitwi hivyo.
Kwa ujumla hili ni neno ambalo hutumika kuelezea watoto ambao wazazi wao walifariki kabla ya wao kufikia umri wa kujitegemea.