Jina la utani | Yanga (Swahili) |
---|---|
Imeanzishwa | 11Feb 1935 |
Uwanja | Benjamin Mkapa National Stadium (Uwezo: 62,000) |
Mwenyekiti | Mshindo Msola |
Meneja | Senzo Mazingiza |
Kocha | Nasreddine Nabi |
Ligi | Tanzania Premier League, Vodacom Premier League |
Tovuti | tovuti ya klabu |
Young Africans S.C. (maarufu kama Yanga, jina kamili ni Young Africans Sports Club) ni timu ya soka ya nchini Tanzania iliyoanzishwa mnamo mwaka 1935, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Jina la utani Timu ya Wananchi au Wanajangwani.
Imepata kuwa mabingwa mara 30 nchini na mabingwa mara 5 kombe la mabingwa Afrika Mashariki Kagame.[1]
Katika ngao ya jamii Yanga imeifunga Azam FC kwa jumla ya magoli 8 kwa 7, takribani mara tatu kwa Azam FC kukutana na Yanga katika Ngao ya Jamii na Yanga kumfunga Azam kwenye mechi zote tatu.[2]