Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Yuri Gagarin

Yuri Gagarin mwaka 1963.

Yuri Alexeyevich Gagarin (kwa Kirusi Юрий Алексеевич Гагарин; 9 Machi 1934 huko Klushino karibu na Smolensk, Urusi - 27 Machi 1968) alikuwa mwanaanga wa kwanza katika historia yaani mtu wa kwanza aliyefika kwenye Anga-nje.

Alimwoa Valentina Goryachova akawa na mabinti wawili ambao ni Galina na Yelena. Akajiunga na Jeshi la Anga ya Urusi mwaka 1955.

Mwaka 1960 aliteuliwa katika kikosi cha kwanza cha marubani walioandaliwa kurushwa kwa anga-nje akateuliwa kuwa mtu wa kwanza wa kutoka duniani.

Tarehe 12 Aprili 1961 alirushwa na chombo cha angani Vostok 1 akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108.[1]

Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo cha kuandaa wanaanga Warusi. Mwaka 1968 alikufa katika ajali ya ndege alipofanya mazoezi ya urubani akazikwa kwenye makaburi ya heshima huko Moscow.

Kuhusiana na kifo Cha Gagarin, maombolezo ya kitaifa yalitangazwa katika Umoja wa Kisovyeti (kwa mara ya kwanza katika historia ya USSR kwa kumbukumbu ya mtu ambaye hakuwa mkuu wa nchi). Kwa heshima ya cosmonaut ya Kwanza Ya Dunia, idadi ya makazi yalipewa jina, barabara na njia zilipewa jina. Makaburi mengi ya Gagarin yamejengwa katika miji tofauti ya ulimwengu.

  1. Wilson, Jim (2011-04-13). "Yuri Gagarin: First Man in Space" (kwa Kiingereza). NASA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-14. Iliwekwa mnamo 2023-03-27.

Previous Page Next Page