Ziwa Ontario ni moja kati ya maziwa makubwa ya Amerika ya Kaskazini. Ziwa limepakana na Kanada (Ontario) upande wa kaskazini halafu na Marekani (New York) upande wa kusini.
Jina la Ontario latoka katika lugha ya Kihurona likimaanisha ziwa kubwa.
Ziwa Ontario hupokea maji yake kutoka Ziwa Erie kupitia Mto Niagara. Maji hutoka kwa nia ya Mto Saint Lawrence.
Majiji mawili makuu ni Toronto (Ontario, Kanada) na Rochester (New York, USA).