Ziwa Superior (yaani Ziwa Kubwa) ni moja kati ya maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini. Ni ziwa kubwa zaidi la bara hili. Pamoja na maziwa ya Ziwa Huron, Ziwa Erie na Ziwa Ontario liko mpakani kati ya Marekani na Kanada na mpaka huo umepita ziwani.
Ziwa limepakana na Kanada (Ontario) upande wa kaskazini halafu na Marekani (Minnesota, Wisconsin na Michigan) upande wa kusini.
Ziwa Superior hupokea maji yake kutoka mito mingi inayoishia humo; maji yake hutoka kwenda Ziwa Huron kupitia mto St. Mary's na Soo Locks.