Abesi

Eufemia Szaniawska, Abesi wa Nieśwież, 1768 hivi, Warsaw.


Ngao ya abesi.

Abesi (kutoka Kiingereza: abbess; pia: abatisa kutoka Kilatini abbatissa) ni cheo cha mmonaki wa kike anayeongoza monasteri kamili; kwa namna fulani kinalingana na kile cha abati na mara nyingi anavaa kama huyo msalaba kifuani kama ishara ya mamlaka yake.

Abesi ni kwa masista wake mama na mwalimu katika safari ya Kiroho. Kwa ajili hiyo anaongoza sala ya jumuia, anagawa majukumu na anasamehe utekelezaji wa vipengele fulanifulani hasa kwa walio wagonjwa.


Abesi

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne