Jiji la Addis Ababa | |
Mahali pa mji wa Addis Ababa katika Ethiopia |
|
Majiranukta: 9°1′48″N 38°44′24″E / 9.03000°N 38.74000°E | |
Nchi | Ethiopia |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 3,352,000 |
Tovuti: www.addisababacity.gov.et |
Addis Ababa (pia Addis Abeba; kwa Kiamhara አዲስ አበባ, "Ua Jipya"; kwa Kioromo Finfinne) ni mji mkuu wa Ethiopia na wa Umoja wa Afrika.
Ina hadhi ya mji wa kujitawala (ras gez astedader) kama jimbo la Ethiopia.
Mji wenyewe una watu kutoka makabila 80, wakiongea lugha 80, na jamii za Waislamu na Wakristo.
Addis Ababa iko mita 2,500 juu ya usawa wa bahari kwa 9.03° N 38.74° E). [1]
Mwaka 2016, idadi ya wakazi ilikuwa 3,352,000 [2], na kwa hiyo Addis Ababa ndio mji mkubwa nchini.
Eneo hii lilichaguliwa na Malkia Taytu Betul na mji kuanzishwa mwaka wa 1886 na mume wake, Mfalme Menelik II, na sasa mji huu una umma milioni nne, na asilimia nane ya ukuzi wa uchumi.
Mji huu uko kwenye Mlima Entoto na ni makazi maalum ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa. Chuo Kikuu cha Addis Ababa kilijulikana kama Chuo Kikuu cha Haile Selassie I, kutokana na jina la Mfalme wa mwisho wa Ethiopia, ambaye alitoa jumba la mfalme (Jumba Guenete Leul) liwe makao maalum ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa mwaka wa 1961.