Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa

Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa (kwa Kiingereza: International Phonetic Alphabet, kifupi IPA) ni mfumo wa alfabeti unaolenga kuonyesha sauti za lugha zote duniani. Imetungwa na wataalamu wa isimu wanaoshirikiana katika Shirika la Kimataifa la Fonetiki (International Phonetic Association). Inatumiwa na watunga kamusi, walimu na wanafunzi wa lugha za kigeni, wanaisimu na wafasiri kote duniani. Kwa hiyo tunakuta alama zake katika kamusi na mara nyingi pia kwenye makala za Wikipedia.

Msingi wa IPA ni alfabeti ya Kilatini pamoja na herufi za pekee zilizochukuliwa kutoka alfabeti nyingine. Herufi hizo zinaunganishwa na alama za pekee.

Mfano ni alama zinazoonyesha sauti tofauti ambazo mara nyingi zinaonyeshwa kwa herufi "A" ambazo zinaweza kuwa na sauti tofauti katika lugha na lahaja mbalimbali kama vile a   ? , ɐ   ?, ɑ   ?, ɒ   ?, æ   ?, ɑ̃ au ʌ   ? (bofya pembetatu ndogo kwa kusikia sauti).

Orodha ya alama zote za IPA pamoja na sauti inapatikana katika Wikipedia ya Kijerumani hapa "Liste der IPA-Zeichen"

Tangu masahihisho ya mwaka 2005[1] kuna herufi 107 na alama za pekee 56.

  1. "IPA: Alphabet". www.langsci.ucl.ac.uk Archived from the original on 18 April 2015. Retrieved 18 April 2015.

Alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne