Altare au madhabahu ni mahali patakatifu inapotolewa sadaka au ibada.
Mara nyingi altare inapatikana ndani ya hekalu au kanisa.
Katika dini nyingi kuna madhehebu ya kafara, dhabihu au matoleo kwa Mungu au mizimu. Ndiyo sababu panahitajika mahali pa kufaa.
Katika Ukristo altare inatiwa maanani kwa kiasi tofauti kulingana na imani ya madhehebu husika juu ya Ekaristi, iliyo ukumbusho wa sadaka pekee ya Yesu Kristo iliyotolewa msalabani.