Apartheid ni neno la Kiafrikaans linalomaanisha "kuwa pekee" au "utengano". Kwa kawaida hutaja siasa ya ubaguzi wa rangi wa kisheria nchini Afrika Kusini kati ya mwaka 1948 na 1994.
Siasa hiyo ilikuwa na utaratibu wa sheria nyingi zilizolenga kutenganisha watu wa rangi au mbari mbalimbali. Kusudi lake lilikuwa kimsingi kutunza kipaumbele cha makaburu na kuhakikisha Waafrika Weusi wasianze kushindana nao kwenye soko la kazi na nafasi za kijamii.