Bahari Nyeusi

Ramani ya Bahari Nyeusi
Bahari Nyeusi inavyoonekana kutoka angani (NASA)

Bahari Nyeusi ni bahari ya pembeni ya Mediteranea inayozungukwa na nchi kavu pande zote iliyoko kati ya Ulaya ya Mashariki na Asia ya Magharibi. Imeunganishwa na Bahari ya Mediteranea kwa njia ya Bahari ya Marmara pamoja na milango ya bahari ya Bosporus na Dardaneli. Ina eneo la takriban 424,000 km² na kina hadi 2,244 m.

Nchi zinazopakana ni Uturuki, Bulgaria, Romania, Ukraine, Urusi na Georgia. Rasi ya Krim ni sehemu ya kujitawala ya Ukraine.

Miji muhimu mwambaoni ni: Istanbul, Burgas, Varna, Constanţa, Yalta, Odessa, Sevastopol, Kerch, Novorossiysk, Sochi, Sukhumi, Poti, Batumi, Trabzon, Samsun na Zonguldak.


Bahari Nyeusi

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne