Bahari ya Marmara

Bahari ya Marmara

Bahari ya Marmara (Kituruki Marmara denizi, Kigiriki: Propontis) ni gimba la maji ya chumvi kati ya Ulaya na Asia ndani ya nchi ya Uturuki. Imezungukwa na nchi kavu pande zote isipokuwa kuna milango miwili miembamba ya kuiunganisha na [Mediteranea] upande wa kusini na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini. Milango hii ni Dardaneli upande wa Mediteranea na Bosporus upande wa Bahari Nyeusi.

Urefu wake ni hadi 282 km na upana 80 km. Kina cha maji hufikia mita 1,300 chini ya UB. Eneo lake ni 11,655 km² na 182 km² ni visiwa ndani yake.

Mji mkubwa kando yake ni Istanbul.


Bahari ya Marmara

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne