Barack Obama | |
6 Desemba 2012 | |
Aliingia ofisini Januari 20, 2009 | |
Makamu wa Rais | Joe Biden |
mtangulizi | George W. Bush |
aliyemfuata | Donald Trump |
Muda wa Utawala Januari 3, 2005 – Novemba 16, 2008 | |
mtangulizi | Peter Fitzgerald |
aliyemfuata | Roland Burris |
Muda wa Utawala January 8, 1997 – November 4, 2004 | |
mtangulizi | Alice Palmer |
aliyemfuata | Kwame Raoul |
tarehe ya kuzaliwa | Agosti 4 1961 Honolulu, Hawaii, U.S. |
utaifa | American |
chama | Democratic |
ndoa | Michelle LaVaughn Robinson (m. 1992–present) |
mahusiano | Stanley Armour Dunham (grandfather) Madelyn Lee Payne (grandmother) Maya Kassandra Soetoro-Ng (half-sister) |
watoto | Malia Ann Obama (b. 1998) Natasha Obama (b. 2001) |
makazi | Chicago, Illinois |
mhitimu wa | Occidental College Chuo Kikuu cha Columbia (B.A.) Harvard Law School (J.D.) |
Fani yake | Lawyer Professor of constitutional law Community organizer Author |
dini | Ukristo |
Awards | Tuzo ya Nobel ya Amani |
signature | |
tovuti | barackobama.com |
Barack Hussein Obama II (amezaliwa 4 Agosti 1961) alikuwa rais wa 44 wa Marekani. Ni Mwafrika-Mwamerika wa kwanza kushika wadhifa huo, na pia mtu wa kwanza mwenye kuzaliwa Hawaii kuwa rais wa Marekani.
Obama awali alihudumu kama Seneta mdogo kutoka jimbo la Illinois, tangu Januari 2005 hadi alipojiuzulu baada ya kushinda uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2008, mwezi wa Novemba.
Obama alifuzu mwanzo kutoka katika chuo kikuu cha Columbia University, kisha akafuzu katika masomo ya sheria kutoka katika kitivo cha masomo ya sheria kwenye chuo kikuu cha Harvard, ambako alikuwa rais wa jarida la Harvard Law Review.
Alihudumu baadaye kama mwanaharakati wa mambo ya kijamii, kabla ya kuhitimu katika masomo ya kisheria.
Hatimaye, alifanya kazi kama wakili wa haki za umma mjini Chicago, kisha akafunza sheria ya kikatiba katika Chuo Kikuu cha Chicago kuanzia 1992 hadi 2004.
Obama alihudumu mihula mitatu katika Bunge la jimbo la Illinos (Illinois Senate) tangu 1997 hadi 2004. Baada ya kushindwa katika jitihada zake za kuchaguliwa katika Bunge Dogo la Marekani mwaka 2000, Obama alisimama kuchaguliwa katika Bunge La Maseneta La Marekani mwaka 2004. Alishinda uchaguzi hapo Novemba 2004.
Alitangaza kusimama kuchaguliwa kama rais wa Marekani mwezi Februari, mwaka 2007. Baada ya kampeni kali katika uteuzi wa chama cha Democratic Party dhidi ya Hillary Clinton, aliteuliwa kama mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho. Katika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2008, alimshinda John McCain, aliyekuwa ameteuliwa na chama cha Republican Party, akaapishwa kama rais tarehe 20 Januari 2009.
Tarehe 9 Oktoba 2009, Obama alituzwa kwa Tuzo ya Nobel ya Amani.
Mwaka 2012 alishinda tena uchaguzi mkuu na kuendelea kuongoza hadi tarehe 20 Januari 2017, alipompisha Donald Trump.