Bendera ya Ufaransa (Kifaransa: Tricolore = rangi tatu) ina milia mitatu ya kusimama katika rangi za buluu - nyeupe - nyekundu.
Imeanzishwa wakati wa mapinduzi ya Ufaransa kabla ya mwaka 1794. Rangi nyeupe ilikuwa rangi ya kifalme. Rangi za nyekundu na buluu zilikuwa rangi za mji wa Paris. Zote pamoja ziliahi kutumika hata kabla ya mapinduzi lakini bila utaratibu maalumu.
Mbunge La Fayette alianzisha alama ya rangi hizi tatu zikikaa kama mviringo kama kitambulisha cha mapinduzi.
Mwaka 1794 Buge ilitangaza bendera hii kuwa bendera rasmi ya taifa.