Bibi kwa mjukuu wake ni hasa mama wa mzazi wake mmojawapo. Katika DNA anachangia 25%.
Inakadiriwa kwamba miaka 30,000 iliyopita idadi ya watu waliofikia umri wa kuona wajukuu wao iliongezeka sana na kuwezesha ushirikishaji wa ujuzi na mang'amuzi mbalimbali kuliko awali.[1][2]
Pia bibi anaweza kushika nafasi ya mama ikiwa huyo hayupo (k.mf. amekufa) na kumfaidisha mtoto kimalezi. Hata kama mama yupo, bibi anaweza kutoa mchango mzuri katika makuzi ya mtoto.
Mwanamke aliyewahi kuliko wote kupata mjukuu ni Rifca Stănescu, a gypsy wa Romania, aliyejifungua mara ya kwanza akiwa na miaka 12, halafu binti yake Maria alizaa akiwa na miaka 11 tu, akimfanya hivyo Rifca kuwa bibi akiwa na miaka 23.[3][4][5][6]