Jiji la Bogota | |
Nchi | Kolumbia |
---|---|
Tovuti: www.bogota.gov.co |
Bogota (jina kamili: Santa Fe de Bogotá) ni mji mkuu wa Kolombia pia mji mkubwa wa nchi mwenye wakazi milioni saba takriban.
Mji uko katika nyanda za juu kwenye kimo cha 2,640 m juu ya UB kati ya milima ya Guadalupe (3,317 m) na Monserrate (3,100 m).
Mji ulianzishwa na Mhispania Gonzalo Jiménez de Quesada tar. 6 Agosti 1538 kwenye mahali pa soko la Wachibcha lililoitwa "Bacata". Quesada alitumia jina la "Santa Fe" (kihisp.: "imani takatifu") kutokana na mji wa Hispania alikotokea mwenyewe.
Baadaye mji uliongezewa jina la pili "Bogota" kutokana na jina asilia "Bacata". Jina kamili lilikuwa "Santa Fe de Bogota".