Britania

Makala hii kuhusu "Britania" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Kisiwa cha Britania kati ya Ueire (Ireland) na Ulaya bara

Britania ni kisiwa kikubwa cha Ulaya chenye eneo la 229,850 km² pia kisiwa kikubwa cha nane duniani. Kwenye kisiwa hiki kuna nchi tatu za Uingereza, Welisi na Uskoti.

Britania iko katika Atlantiki kati ya Bahari ya Ueire (Ireland) na Bahari ya Kaskazini. Pamoja na visiwa vya Ueire (Eireland), Faroe, Isle of Man Man na visiwa vingi vidogo ni sehemu ya funguvisiwa ya Britania.

Britania huteganishwa na Ulaya bara kwa Mfereji wa Kiingereza. Mji wa Dover katika Uingereza ya kusini una umbali wa 34 km na mji wa Calais katika Ufaransa.

Jina la Britania limetokana na Waroma wa Kale waliovamia kisiwa na kufanya sehemu ya kusini kuwa jimbo la dola lao. Jimbo la Britania ya Kiroma liliunganisha nchi za Uingereza na Welisi za leo.

Kisiwa chote ni sehemu ya Ufalme wa Muungano unaoitwa mara nyingi "Uingereza" kutokana na nchi kubwa ndani yake. Lakini ufalme huu ni kubwa kushinda Britania, uko pamoja na Eire ya Kaskazini, visiwa vya Hebridi, Orkney na Shetland, halafu maeneo ya ng'ambo. Hizi zote si sehemu ya Britania lakini ziko pamoja katika Ufalme wa Muungano.

Visiwa katika mfereji wa Kiingereza na kisiwa cha Isle of Man viko chini ya malkia au mfalme wa Uingereza lakini si sehemu za Ufalme wa Muungano.

Britania huitwa pia "Britania Kuu" kwa sababu ya "Britania ndogo" katika Ufaransa (Kiingereza: "Brittany"; Kifaransa: "Bretagne").

Mara nyingi neno la "Uingereza" linatumiwa kutaja kisiwa chote kwa sababu Uingereza ni nchi kubwa kisiwani.


Britania

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne