Kata ya Bulongwa | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Njombe |
Wilaya | Makete |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 3,517 |
Bulongwa ni makao makuu ya Wilaya ya Makete katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59514.
Bulongwa iko kwenye sehemu ya magharibi ya milima ya Livingstone kwenye kimo cha mita 2,100 juu ya UB. Hakuna joto kali, tena wakati wa Juni - Agosti jalidi hutokea. Mvua unatokea kati ya Novemba hadi Mei.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 3,517 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,824 [2] walioishi humo.
Mji huo ni kitovu cha dayosisi ya kusini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Kati, kuna hospitali ya kanisa na ofisi za dayosisi.