Buluu

Buluu/Bluu
( #0000FF)


Buluu ni moja ya rangi za pinde ya mvua. Inahesabiwa kati ya rangi kuu zinazoonekana kwa macho ya binadamu oamoja na nyekundu na manjano.

Buluu ni rangi ya anga ikiwa bila mawingu wakati wa mchana jua likiwaka. Wakati huu ni pia rangi ya bahari na maziwa makubwa yanayoakisisha rangi ya anga.

Dunia ina pia rangi ya buluu ikitazamiwa na wanaanga kutoka anga-nje.


Buluu

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne