Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.
Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini[1].
Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.
Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio,pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili[2]
Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya[3]. Kinga ni bora kuliko tiba.