Dari (kwa Kiing. ceiling) ni sehemu inayofunika kikomo cha juu cha chumba .
Inaficha tu paa juu yake au sehemu ya chini ya sakafu ya ghorofa ya juu.
Kuna aina nyingi tofauti za dari katika usanifu majengo.
Kuna dari tambarare na kuna dari yenye umbo la kuba. Katika majengo ya kisasa, mara nyingi dari ni uso wa chini wa sakafu ya ghorofa ya juu.
Katika majengo ya kidini, dari mara nyingi hupambwa kwa michoro au mozaiki. Mfano maarufu ni dari ya Kikanisa cha Sisto IV iliyochorwa na Michelangelo.