Douala ni mji mkubwa wa Kamerun ukiwa na wakazi 1,338,082 (2021[1]).
Uko kilometa 24 kutoka bahari kwenye mdomo mpana wa mto Wouri unaokomea kwenye Ghuba ya Guinea ya Atlantiki. Bandari yake inaifanya kuwa kitovu cha uchumi wa Kamerun.
Wakati wa ukoloni wa Kijerumani ulikuwa mji mkuu wa Kamerun hadi mwaka 1907.