Elimu nchini Côte d'Ivoire inaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi. Kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika kwa watu wazima bado kipo chini: mnamo 2000, ilikadiriwa kwamba 48.7% ya jumla ya wakazi wanajua kusoma na kuandika (60.8% ya wanaume na 38.6% ya wasichana). [1] Watoto waliowengi kati ya miaka 6 na 10 hawajaandikishwa shule. [2] Idadi kubwa ya wanafunzi wa elimu ya sekondari ni wanaume.[3] Mwishoni mwa elimu ya sekondari, wanafunzi wanakaa na kufanya mtihani wa mwisho (Baccalauréat).[3] Nchi ina vyuo vikuu mjini Abidjan (Université de Cocody) na huko Bouaké, (Université de Bouaké).