Fonetiki (kutoka Kiingereza "Phonetics") ni tawi la sayansi ya isimu. Inashughulikia uchunguzi wa sauti za lugha za binadamu, pamoja na utamkaji na usikiaji wake. Kwa ujumla, fonetiki ni tawi la isimu linalochunguza jinsi sauti zinavyozalishwa, zinavyosafirishwa na zinavyomfikia msikilizaji.
Etimolojia ya neno fonetiki imebeba dhana mbili: foni na etiki. Foni humaanisha sauti, ilihali etiki ni dhana pana kidogo.
Vitamkwa huandikwa kwa kutumia alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa (au kifupi cha jina lake kwa Kiingereza, International Phonetic Alphabet).
Fonetiki inagawanyika katika: