Habari (kutoka Kiarabu) ni mawasiliano ya maarifa kuhusu matukio ambayo huwasilishwa kwa watu kwa maneno ya kinywa, kwa maandishi kama vile magazeti, kwa matangazo ya masafa marefu kama vile redio au runinga, kwa intaneti n.k.
Neno hili linaweza kutumiwa pia katika sayansi kwa mawasiliano ya habari (kwa Kiingereza information, si news) kati ya seli za mwili, kwa mfano kati ya mkono na ubongo, kwa njia ya neva.