Harvard Law Review ni jarida la kisheria lenye kufuatilia habari za kisheria na maamuzi ya Mahakama za Marekani. Jarida hili huchapishwa na wanafunzi katika kitivo cha Sheria kwenye chuo Kikuu cha Harvard kila mwezi kuanzia Novemba hadi Juni.
Jarida hili lilichapishwa mara ya kwanza 15 Aprili 1887, na lina wahariri wakuu 14 wanaochaguliwa kila mwaka kutoka katika ujumla wa wanafunzi katika kitivo hicho cha sheria.