| |||||
Lugha rasmi | Kisango, Kifaransa | ||||
Mji Mkuu | Bangui | ||||
Mji Mkubwa | Bangui | ||||
Serikali | Jamhuri | ||||
Rais | Faustin-Archange Touadéra | ||||
Eneo | km² 622,984 | ||||
Idadi ya wakazi | 3,895,139 (2018) | ||||
Wakazi kwa km² | 6.25 | ||||
Uchumi nominal | Bilioni $2.003 | ||||
Pesa | CFA frank (XFA) (Frank ya Afrika ya Kati) | ||||
Kaulimbiu | "Umoja, Heshima, Kazi" | ||||
Wimbo wa Taifa | E Zingo (Uamsho mpya) | ||||
Jamhuri ya Afrika ya Kati (kwa Kisango Ködörösêse tî Bêafrîka) ni nchi ya bara bila pwani katika Afrika ya Kati.
Imepakana na Chadi upande wa kaskazini, Sudan na Sudan Kusini upande wa mashariki, Jamhuri ya Kongo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa kusini na Kamerun upande wa magharibi.