Jimbo la Morogoro (kwa Kilatini: Dioecesis Morogoroensis) ni mojawapo katika ya majimbo 35 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania kwa ajili ya waumini wake katika manispaa ya Morogoro pamoja na wilaya za Bagamoyo, Morogoro vijijini, Mvomero, Kilosa, Gairo n.k.
Eneo lote lina kilometa mraba 43,380.
Kutokana na historia yake linafuata mapokeo ya Kanisa la Kiroma, kama majimbo mengine yote ya Tanzania.