Anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayoonekana kuathiri dunia hadi leo.
Baadhi ya mafanikio hayo ni:
Kama kiongozi wa kijeshi aliteka Gallia (leo: Ufaransa) na kuifanya jimbo la Kiroma. Kutokana na hiyo lugha ya Kifaransa ni karibu sana na Kilatini, lugha ya Roma ya Kale.
Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kutangulia akatangazwa kuwa mungu. Jina lake lilipata kuwa neno kwa ajili ya cheo cha watawala wa Kiroma waliomfuata. Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama vile Kijerumani ("Kaiser"), Kirusi ("Tsar") na Kiswahili ("Kaisari" - kutokana na neno la Kijerumani).
↑Kwa matamshi ya Kilatini sanifu cha Kale herufi "C" ilikuwa na matamshi ya "K"; katika matamshi ya karne za baadaye ilikuwa zaidi "Ch" kwa hiyo "Chesar"; kutoka hapo yametokea matamshi ya Kiingereza "Sizar"