Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika (kwa Kiingereza: African Economic Community, kifupi: AEC) ni muundo wa nchi za Umoja wa Afrika ambao unaweka misingi ya maendeleo ya pamoja kati ya nchi zilizo nyingi za Afrika.
Jumuiya ilianzishwa kwa Abuja Treaty, iliyosainiwa mwaka 1991 na kuanza kufanya kazi mwaka 1994.
Kupitia hatua sita, malengo ni kuanzisha maeneo ya biashara huru, miungano ya forodha, soko la pamoja, benki kuu na pesa ya pamoja (African Monetary Union) hadi kufikia muungano katika uchumi na pesa mwaka 2028 na kukamilisha mpango mzima kabla ya mwaka 2034.