Kamera

Kamera
Kamera.
Kamera ya kidijitali.

Kamera ni kifaa kinachochukua picha. Ina tundu moja dogo tu kwa kupokea nuru inayoacha picha ndani yake ama kwenye filamu au kwenye kihisio elektroniki. Kwa kawaida nafasi hii huwa na lenzi inayozalisha picha ya yale yaliyo nje.

Kamera tuli hushika picha moja-moja. Picha zinazopigwa mfululizo, angalau picha 15 kwa sekunde au zaidi, zinaweza kushika mwendo utakaoonekana baadaye kama filamu kama picha hizi zinaonyeshwa mfululizo kwa kutumia projekta au kwenye skrini ya sinema runinga au kompyuta.

Kamera zote kimsingi ni sanduku inayofungwa pande zote. Nuru haiwezi kuingia mpaka kilango kinafunguliwa n kupitisha nuru kwa kipindi kifupi cha sehemu ya sekunde pekee. Kilango hiki kipo nyuma ya lenzi. Kwa upande mwingine ni wenzo maalum ambao unaweza ku rekodi pichaambayo inakuja kupitia lenzi. Wenzo huu ni filamu katika kamera ya filamu au kihisio elektroniki katika kamera dijiti.

Wakati picha inachukuliwa, kilango kinatoka nje ya njia. Hii inawezesha nuru kuingia kwa njia ya lenzi na kuzalisha picha kwenye filamu au kihisio elektroniki. Katika kamera nyingi, ukubwa wa tundu unaweza kubadilishwa kulingana na mwangaza au giza ya mazingira. Muda ambao kifuniko kinauwezesha mwanga inaweza pia kubadilishwa. Hii pia inakuwezesha mwanga zaidi au mwanga mdogo. Mara nyingi, umeme ndani ya kamera hudhibiti haya, lakini katika kamera nyingine mtu anayeichukua picha anaweza kubadilisha pia.

Lenzi humwezesha mpigapicha kuvuta mbali au karibu anayoipiga. Kwa njia hii mpigapicha anapata uwezo wa kupiga kwa urahisi picha ya kitu kilicho mbali au kitu kidogo sana na kupata picha safi.

Kamera nyingi huwa na lenzi yake na uwezo wa kuongezewa lenzi nyingine ya nje kulingana na kazi inayolengwa kufanywa. Lenzi za nje zina uwezo na urefu wa kuona tofauti kulingana na ukubwa wake na idadi ya lenzi zinazotumika. Kuna lenzi za nje za kamera za simu pia.


Kamera

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne