Kaunti ya Taita-Taveta | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kaunti | |||||
| |||||
Taita-Taveta County in Kenya.svg Kaunti ya Taita-Taveta katika Kenya | |||||
Nchi | Kenya | ||||
Namba | 6 | ||||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Pwani | ||||
Makao Makuu | Mwatate | ||||
Miji mingine | Voi, Wundanyi, Taveta | ||||
Gavana | Granton Graham Samboja | ||||
Naibu wa Gavana | Majala Mlagui Delina | ||||
Seneta | Johnes Mwashushe Mwaruma | ||||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Lydia Haika Mnene Mizighi | ||||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Taita-Taveta | ||||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 20 | ||||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 4 | ||||
Eneo | km2 17 152 (sq mi 6 622) | ||||
Idadi ya watu | 340,671 [1] | ||||
Wiani wa idadi ya watu | 20 | ||||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||||
Tovuti | taitataveta.go.ke |
Kaunti ya Taita-Taveta ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Imepakana na Kaunti za Kwale, Kitui, Kilifi, Tana River, Kajiado na Makueni. Pia, imepakana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makao makuu yako Mwatate.
Idadi ya watu waliohesabiwa katika sensa iliyofanywa mwezi wa Agosti 2019 ni 340,671 katika eneo la km2 17,152, msongamano ukiwa hivyo wa watu 20 kwa kilometa mraba[2].[3].
Taita-Taveta ina mbuga za wanyama za Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi.
Ziwa Jipe na Ziwa Chala hupatikana katika kaunti hii katika mpaka wa Kenya na Tanzania.