Kaunti ya Tana River | |
---|---|
Kaunti | |
Tana River County in Kenya.svg Kaunti ya Tana River katika Kenya | |
Coordinates: 1°30′S 40°0′E / 1.500°S 40.000°E | |
Nchi | Kenya |
Namba | 4 |
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 |
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Pwani |
Makao Makuu | Hola |
Miji mingine | Madogo |
Gavana | Dhadho Gaddae Godhana |
Naibu wa Gavana | Kea Batuyu Salim |
Seneta | Golich Juma Wario |
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Rehema Hassan |
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Tana River |
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 15 |
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 3 |
Eneo | km2 39 950.5 (sq mi 15 425.0) |
Idadi ya watu | 893,681[1]. |
Wiani wa idadi ya watu | 8 |
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) |
Tovuti | tanariver.go.ke |
Kaunti ya Tana River ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 893,681 katika eneo la km2 39,950.5, msongamano ukiwa hivyo wa watu 8 kwa kilometa mraba[2]. Kabila kuu ni Wasomali (pamoja na Wawardey, ambao kwa asili ni Waoromo) halafu Wapokomo, ambao wengi ni wakulima, na Waorma, ambao hutegemea ufugaji wa kuhamahama.
Mji wa Hola ndio makao makuu ya serikali ya kaunti na ndio mji mkubwa zaidi.
Jina lake limetokana na Mto Tana.
Kwa jumla, kaunti hiyo ni kavu na huwa na ukame. Mvua si za hakika, msimu wa mvua huja miezi za Machi-Mei na Oktoba-Desemba. Kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji wahamaji juu ya maji. Mafuriko pia ni tatizo la kawaida, yakisababishwa na mvua nzito katika maeneo ya juu ya Mto Tana.
Kaunti ya Tana inajumuisha maeneo kadhaa ya misitu, vichaka na mapori ambayo ni maeneo madogo ya makazi. Misitu huteuliwa kama Hifadhi ya Kitaifa ikiwa ina zaidi ya aina nne za mimea mikuu na zaidi ya aina saba za wanyama wakubwa (IUCN, 2003).
Licha ya udhahiri wa maliasili ya kutosha, eneo hili bado limetengwa katika maeneo mengine ya nchi. Juhudi za maendeleo daima huzunguka eneo kubwa la Mto Tana, licha ya kutokuweko kwa mafanikio katika miradi ya awali ya kunyunyisha maji katika wilaya, yaani, miradi za kunyunyishia maji za Bura, Hola na mradi wa kukuza mpunga wa Tana delta ambao haukufanikiwa baada ya kuharibiwa na maji ya mvua za El Nino mwaka wa 1998.
Utafiti ulioandaliwa na ALMRP, Wilaya ya Mto Tana na kukabidhiwa kwa Kamati ya Maendeleo ya Wilaya ya Tana River (2004), iligundua kuwa kaunti hiyo ilikuwa na 79% ukosefu wa chakula na huku kiwango cha umaskini kikifika hadi 62% [3].