Kiafar ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Ethiopia, Eritrea na Jibuti inayozungumzwa na Waafar. Mwaka wa 1994 idadi ya wasemaji wa Kiafar nchini Ethiopia imehesabiwa kuwa watu 906,000. Pia kuna wasemaji 99,200 nchini Jibuti (2006). Idadi ya Waafar nchini Eritrea haijulikani. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiafar iko katika kundi la Kikushi.