Kiarmenia ni lugha ya pekee katika jamii ya lugha za Kihindi-Kiulaya.
Kinatumiwa na watu milioni 6, hasa nchini Armenia (ambapo ni lugha rasmi) na kandokando yake.
Alfabeti yake maalumu ilibuniwa na Mesrop Mashtots mwaka 405.
Fasihi yake ina historia ndefu, ikianza na tafsiri ya Biblia ya karne ya 5.