Kichochezi (pia kichocheo, kwa Kiing. catalyst) ni istilahi ya kemia inayotaja dutu ambayo hubadilisha kasi au kima cha mmenyuko wa kikemia (au utendanaji, Kiing. reaction) na yenyewe isiathiriwe wala kubadilika mwanzo hadi mwisho[1].
Mfano wake ni ukitia oksidi ya manganisi (MnO2) kwenye peroksidi ya hidrojeni (H2O2) ambayo itaanza haraka kuvunjika kuwa maji na oksijeni, ilhali MnO2 inabaki.
Kichochezi ndani ya michakato ya kikemia ya mwili huitwa kimeng'enya.
Kinyume chake ni kiviza, yaani dutu ambayo huzuia au hupunguza mwendo wa mmenyuko.