Kidole cha kati cha kando (pia: kidole cha pete) ni kidole cha nne mkononi. Iko kati ya kidole kikubwa na kidole cha mwisho.
Kidole hiki hakina nguvu sana ni hafifu kati ya vidole vingine kwa sababu ya mishipa yake ni michache.
Katika tamaduni za magharibi kinatumiwa kwa ajili ya pete ya ndoa. Wengine hutoa maelezo juu ya imani mbalimbali kama sababu ya desturi hiyo. Labda sababu ya kimsingi ni udhaifu wa kidole hiki: kama ni kidhaifu kati ya vidole hakitumiwi sana kwa kazi kama kidole gumba au kidole cha shahada. Hivyo pete inalindwa zaidi ikiwa kwenye kidole hiki kuliko kwenye kidole kingine.
Kuna lugha kadha ambako kidole hiki huitwa kwa majina kama "kidole cha daktari".
Katika Kirusi, Kifinland na Kituruki kuna imani ya kwamba kidole hiki kina uhusiano na uchawi.
Sehemu za Mkono wa binadamu | ||
---|---|---|
Bega * Mkono wa juu * Kisugudi * Kigasha * Kiganja * Kidole gumba * Kidole cha shahada * Kidole cha kati * Kidole cha pete * Kidole cha mwisho |