Kifua Kikuu | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Infectious diseases, pulmonology |
ICD-10 | A15.–A19. |
ICD-9 | 010–018 |
OMIM | 607948 |
DiseasesDB | 8515 |
MedlinePlus | 000077 Kigezo:MedlinePlus2 |
eMedicine | med/2324 |
MeSH | D014376 |
Kifua kikuu (kwa Kiingereza tuberculosis, kifupi TB) ni ugonjwa wa kuambukizwa ulio hatari. Ugonjwa huu husababishwa na aina mbalimbali za bakteria ambazo hujulikana kama Mycobacterium tuberculosis.[1]
Kifua kikuu kwa kawaida kinaathiri mapafu, lakini pia kinaweza kuathiri sehemu nyingine za mwili.
Kifua kikuu husambazwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kupitia hewa wakati anapokohoa, kupiga chafya, au mate yake yakiwa hewani[2]
Maambukizi mengi hayana dalili wala hayaleti madhara. Lakini moja kati ya maambukizo kumi yasiyoleta madhara hatimaye huendelea na kuwa ugonjwa kamili. Kama kifua kikuu kisipotibiwa, kinaua zaidi ya 50% ya watu walioambukizwa.
Dalili za kawaida za maambukizi ya kifua kikuu kinacholeta madhara ni kikohozi sugu na kukohoa damu, Kohozi, homa, kutokwa na jasho usiku, na kukonda. Maambukizi ya viungo vingine husababisha dalili mbalimbali. Njia ya kitaalamu ya utambuzi wa kifua kikuu kwa kutumia eksirei ya kuchunguza ugonjwa hujulikana kama eksirei ya kifua na pia wanatumia hadubini na kufanya uchunguzi wa vimelea maradhi vya majimaji ya mwilini. Uchunguzi wa kifua kikuu kisicholeta madhara hutumia kipimo kiitwacho kipimo cha ngozi (TST) na vipimo vya damu.
tiba si rahisi na inabidi kupewa dawa nyingi za kinga mwili kwa kipindi kirefu. Mawasiliano ya kijamii pia yanapimwa na kutibiwa kama inavyotakiwa. Dawa zinazoshindwa kutibu magonjwa ni tatizo kubwa la maambukizi sugu mengi ya kifua kikuu]] (MDR-TB).
Ili kuzuia kifua kikuu, ni lazima watu wapimwe ugonjwa na wapate chanjo ya bacillus Calmette - Guérin.
Wataalamu wanaamini kwamba theluthi moja ya idadi ya watu duniani waliambukizwa kifua kikuu,[3] na kila sekunde kuna mtu ambaye anaambukizwa [3]. Mwaka 2007, kadri ya watu 13,700,000 duniani waliambukizwa kifua kikuu kinacholeta madhara sugu. Mwaka 2010, kadri ya milioni 8.8 ya watu waliambukizwa na milioni 1.5 ya watu walifariki baada ya kuambukizwa na kifua kikuu, na wagonjwa wengi wanapatikana katika nchi zinazoendelea.[4] Idadi halisi ya wagonjwa wa kifua kikuu imekuwa ikipungua tangu mwaka 2006, na kesi mpya zimeshuka tangu mwaka 2002.[4]
Kifua kikuu si ugonjwa unaosambazwa sawasawa duniani kote. Kadri ya 80% ya watu katika nchi nyingi za Asia na Afrika waliofanyiwa kipimo cha ngozi walionekana wameambukizwa, lakini ni asilimia 5-10% tu ya wananchi wa Marekani ambao walionekana na ugonjwa huo.[1] Watu wengi waliopo katika nchi zilizoendelea wanaambukizwa kifua kikuu kwa sababu ya kutokuwa na kinga. Kwa kawaida, hawa watu wanaambukizwa kifua kikuu baada ya kuambukizwa na VVU na hatimaye wanapatwa na UKIMWI.[5]
{{cite book}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
<ref>
tag; no text was provided for refs named Lancet11