Kikorsika (Corsu au lingua corsa) ni mojawapo ya lugha za Kirumi inayotumika na watu wasiopungua 150,000, hasa katika visiwa vya bahari ya Tireni. Inafanana sana na Kiitalia, hasa lahaja ya mkoa wake wa Toscana[1], kiasi kwamba wengine wanakiona Kikorsika kuwa lahaja, si lugha ya pekee.
Jina linatokana na kisiwa cha Korsika ambapo ilikuwa lugha ya kawaida hadi karne ya 20, ilipozidiwa na Kifaransa kiasi kwamba inaelekea kufa[2]. Kumbe inaendelea vizuri zaidi kaskazini mwa kisiwa jirani, Sardegna (Italia).