Kimachinga ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wamachinga. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kimachinga imehesabiwa kuwa watu 36,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kimachinga iko katika kundi la P20.