Kimambwe-Lungu ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania na Zambia inayozungumzwa na Wamambwe, Walungu na Wafipa. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kimambwe-Lungu nchini Tanzania imehesabiwa kuwa watu 295,000 ambao 230,000 wao wlaikuwa Wafipa walioongea Kimambwe badala ya lugha yao ya Kifipa. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kimambwe-Lungu iko katika kundi la M10.