Kinasasauti

Kinasasauti ya miaka ya 55s

Kinasasauti (pia mikrofoni au maikrofoni kutoka lugha ya Kiingereza: microphone) ni kifaa kinachoweza kuichukua sauti na kuibadili ili iwe ishara za umeme (electrical signals).

Kinasasauti hutumika katika simu, vifaa vinavyosaidia watu walio na shida za kusikia, pamoja na vifaa vya kuhadhiri kwa watu wengi katika jukwaa na ukumbi. Unapoongea kwa kinasasauti, ile sauti hufanywa kubwa na baadaye kusikika kwa kipaza sauti. Kinasasauti pia hupatikana katika studio za kurekodi muziki ambapo mtu hukitumia na ile sauti huhifadhiwa kwa tarakilishi na baadaye kuhaririwa ili muziki utolewe. Kwa leo, hili ni jambo la kawaida haswa kwa wale wanaotengeneza video za youtube ili sauti yao iwe ya kuvutia na kusikika kwa urahisi.


Kinasasauti

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne