Kingasa (au Kiongamo) ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Tanzania inayozungumzwa na Wangasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kingasa kiko katika kundi la Kinilotiki.
Mwaka wa 1983 idadi ya wasemaji wa Kingasa imehesabiwa kuwa watu 200 tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa. Ingawa kulikuwa na Wangasa zaidi ya 4,000 mwaka wa 2000, wengi walikuwa wameshasahau lugha yao na kutumia Kimaa, Kichaga au lugha nyinginezo. Inawezekana kwa sasa hakuna anayejua tena Kingasa.