Kwa lugha ya Kiselti, angalia makala ya Kigaeli cha Uskoti.
Kiskoti ni mojawapo ya lugha za Kianglia, kundi la lugha zinazofanana sana na Kiingereza hata kama ni lugha tofauti. Kama Kiingereza, Kiskoti ni lugha ya Kijerumaniki Magharibi, lakini Kiskoti husemwa hasa nchini Uskoti na kaskazini mwa Eire.[1]
Kiskoti ni tofauti na Kigaeli cha Uskoti, lugha ya Kiselti ambayo mara nyingi inachanganyika na Kiskoti. Pia ni tofauti na Kiingereza cha Uskoti, lahaja ya Kiingereza nchini Uskoti.