Kitausug (pia Kisulu) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Ufilipino, Malaysia na Indonesia inayozungumzwa na Watausug kwenye visiwa vya Palawan, Basilan na Kalimantan. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kitausug imehesabiwa kuwa watu 900,000 nchini Ufilipino na watu 150,000 nchini Malaysia. Pia kuna wasemaji 12,000 nchini Indonesia (1981) Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kitausug iko katika kundi la Kifilipino.