Kitaveta ni lugha ya Kibantu nchini Kenya inayozungumzwa na Wataveta. Wataalamu wengine huiangalia kama lahaja ya Kitaita.
Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kitaveta imehesabiwa kuwa watu 21,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kitaveta iko katika kundi la G20.
Lugha ya Kitaveta inafanana kwa zaidi ya asilimia 95 (95%) na lugha ya Kipare inayotumika nchini Tanzania.