Kiurdu (pia hujulikana kama Lashkari imeandikwa لشکری[1]) ni aina ya lugha ya Kihindi iliyosanifiwa.
Ndiyo lugha rasmi ya Pakistan na ya majimbo 6 ya India (katika nchi hiyo ni mojawapo kati ya 22 zinazokubaliwa na katiba).
Kwa kawaida kinaandikwa kwa herufi za Kiarabu kutokana na uhusiano wake na dini ya Uislamu.
Wanaokitumia kama lugha mama ni watu milioni 65.