Kivietnam ni lugha ya Kiaustro-Asiatiki nchini Vietnam, Kamboja na Uchina inayozungumzwa na Wavietnam. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kivietnam imehesabiwa kuwa watu milioni 65.8 nchini Vietnam na 7200 nchini Uchina. Pia kuna wasemaji 72,800 nchini Kamboja. Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kivietnam iko katika kundi lake lenyewe la Kivietnam.
Lugha ya Kivietnam ni lugha rasmi nchini Vietnam. Pia huzungumzwa katika nchi nyingi na wahamiaji Wavietnam, k.m. Marekani, Australia na nchi za Ulaya.