Kiyoruba ni lugha ya Kiniger-Kongo hasa nchini Nigeria inayozungumzwa na Wayoruba. Ni lugha rasmi mojawapo ya nchi ya Nigeria. Mwaka wa 1993 idadi ya wasemaji wa Kiyoruba nchini Nigeria imehesabiwa kuwa watu karibu milioni 19. Pia kuna wasemaji 465,000 nchini Benin. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiyoruba iko katika kundi la Kidefoidi.